Friday, November 15, 2013

MASTAA WASHIKANA UCHAWI...WANYOOSHEANA VIDOLE WAO KWA WAO.


Stori:Musa Mateja.
Tuhuma za mastaa wa Bongo kujihusisha na mambo ya Ulozi au Uchawi imeibuka upya na safari hii bundi kajikita zaidi kwenye kiwanda cha Sinema za Kibongo.
Ijumaa linaripoti kamili.

UCHUNGUZI:
Uchunguzi wa gazeti hili ndani ya ulimwengu wa mastaa hao ulibaini kwamba,ukiwaacha wale wa Bongo Fleva ambao wamekuwa wakishikana uchawi kila kukicha,kwenye filamu ndiko hakufai kabisa.

Ilibumburuka kwamba maswala ya kulogana ndiyo yamesababisha filamu za baadhi yao kudoda na kukosa soko.
Inaelezwa kwamba mbali na sinema zao kubuma wamekuwa wakizibiana riziki za tenda kama ilivyokuwa zamani.

KIVIPI?
Kwa mujibu wa 'mtaalam' wao mwenye kituo cha kazi huko Yombo-Buza,Dar,wanachokifanya ni kufifiza na kuzimana nyota hivyo kumpotezea mhusika mvuto kwenye jamii.
“Unajuwa kuna mastaa walikuwa na majina makubwa lakini siku hizi siyo kama zamani.

“Baadhi wanawaroga wenzao kwa kuwasababishia matatizo ya magonjwa au kwenye familia”,alisema mmoja wa wasanii waliokuwa wakiang'ara zamani lakini siku hizi kafifia huku akimtolea mfano mwigizaji mmoja wa kiume ambaye mkewe aliwahi kumkuta na hirizi.

Katika uchunguzi huo,baadhi ya mastaa walikuwa wakinyoosheana vidole wao kwa wao huku listi ndefu ya mastaa wanaokesha kwa waganga kuwa maliza wenzao ikianikwa(majina tunayo). Ili kupata uthibitisho wa uchunguzi huo,gazeti lilizungumza na baadhi ya vinara wa filamu za Kibongo ambapo wengi walikiri kukithiri kwa ushirikina kwenye tasnia hiyo.

JACOB STEVEN'JB':Sanaa yoyote ili idumu muda mrefu inahitaji baraka na neema ya Mungu.Sisi tulianza enzi za nyota Ensemble 'Mambo hayo',baadaye ilikuja Kaole Sanaa Group ndipo kukaibuka mapinduzi sisi tukashuka.Mimi siamini mambo ya uchawi ila naamini katika kazi tu,wasanii waache kufanya kazi kimazoea.

Maswala ya uchawi mimi sipendi kuyapa nafasi maana hayo kila sehemu yapo,ninachoweza kusema ni kwamba wasanii wengi wa Bongo hawapo'siriasi'

JACQUELINE WOLPER:Mimi naamini sana katika kazi lakini kwa kuwa Mungu ndiye kanipa jina hili,sina budi kumshukuru yeye ila kama nimelipata kwanjia ya uganga basi nikose kabisa.

ROSE NDAUKA:Uchawi ni inshu inayonisikitisha sana na ukweli wapo mastaa wanaofanya mambo hayo ili wapande.Mimi najuwa Mungu hawezi kuwasadia so nawashauri wafanye kazi, wasihangaike na uchawi kwasababu hauwezi kuwapandisha.

KAJALA MASANJA:Kusema ukweli uchawi unatajwa sana kwenye tasnia ya filamu za Bongo hadi inanifanya kuamini hivyo kwasababu kuna watu kweli wakikuona unang'ara kwenye movi watafanya kila wawezavyo wakushushe tu na hasa kwanjia ya ushirikina.

SINGLE MTAMBALIKE'RICHIE':Mimi asili yangu ni Mwanza so kama unavyojuwavyo watu wa Mwanza ni wachapa kazi,so nipo makini sana na kazi yangu ya filamu na nipo kwenye tasnia kwa miaka 17 na maisha yangu na yafanya ya kawaida tu wala sipendi kujikweza.
Kwa staili hiyo ningetumia nguvu za giza ningekuwa tajiri namba moja hapa nchini maana siri ya kazi yoyote ni kuiheshimu na kujibidiisha.

ELIZABERTH MICHAEL'LULU':Tasnia yetu ya filamu naona kama hatuangalii mbali maana kwa wenzetu wanashindana kikazi na si uchawi kama huku wanaoufikiria kuwashusha wenzao kisa wanaona wanafanya vyema,mimi ninachoweza kusema watu wafanye kazi na washabiki kuangalia nani anafanya nii na kumfanyia mambo kama hayo yasiyojenga maisha.

RUTH SUKA'MADINDA':Mimi sijui sana kama kuna watu wanafanya ushirikina.Ninacho waomba wamtegemee sana Mungu.Kama ukimroga mwenzio ili ashuke basi hata wewe huwezi kufika mbali.

JACQUELINE PENTZEL'JACK CHUZ':Kweli mimi ninaumizwa na watu wanaotumia uchawi kuzima nyota yangu kwasababu kweli wapo wanaofanya hivyo tunawaona hata huko lokesheni wanakamatwa na hirizi. Wengine wanakutwa na matunguri ila mwisho wa siku naomba wajue kuwa nyota na mafanikio huletwa na Mungu na kujibidisha katika kazi hivyo ninachoweza kuwashauri watu kama hao waachane na imani za kishirikina.

SALUM HAJI'MBOTO':Mimi ninachojua watu wanatengeneza muvi kupitia migongo ya wenzao,unakuta mtu anatengeneza sinema lakini anajua kabisa bila kumchezesha fulani hawezi kuuza hivyo anatumia nyota ya mwenzake kuuza filamu yake.

AUNT EZEKIEL:Siamini sana katika kurogana ila wanaotumia njia hizo siamini kama wanafanikiwa kiasi hicho maana uigizaji ni kipaji kutoka kwa Mungu na hakuna awezae kushusha kipaji hicho ila najua uchawi upo na watu wanatumia uchawi kwenye mambo yao.

STEVEN NYERERE:Uchawi haupo kwenye filamu tu hayo yapo hata kwenye siasa.Watu kibao wanatembelea nyota za watu.Wapo wanaoshinda kwa waganga,tunawajua lakini cha msingi wafahamu kuwa hata ukimfanyia mtu kitu gani huwezi kuwa staa.

SALOME NDUMBAGWE MISAYO 'THEA':Mimi naona kama chalenji tu na kinyongo,maana wengi wanaotumia nguvu za giza hawachukui muda mrefu wanashuka wao.Ninachoona waachane na nguvu za giza wamtegemee Mungu.

Baadhi ya waigizaji wengine waliowahi kurogwa na wenzao na pamoja na WEMA SEPETU,BLANDINA CHAGULA'JOHARI',NURU NASSOR'NORA', na wengineo.




Credit:Globle Publishers.

MWIMBAJI MKONGWE SQUEEZER AZILAUMU REDIO KUDIDIMIZA WASANII WAKONGWE.


Squeezer ametoa wimbo mpya uitwao “Mtemi Pesa” aliomshirikisha Belle 9,kama jina la wimbo huo linavyojieleza unazungumzia jinsi pesa inavyo tawala kila kitu.

Akizungumza na kipindi cha Planet Base cha Planet Fm Morogoro,Squeezer ambaye ni kaka wa rapper Wa kike Dataz,amesema baadhi ya vyombo vya habari vinachangia katika kuwadidimiza wasanii wakongwe kutokana na baadhi yao kuwabeba wasanii wapya kutokana na kuwa na masilahi nao.

“Mi nafikiri kuna baadhi ya Media zinadidimiza wakongwe kwa maksudi kwa kuwa wanajuwa wana nguvu hiyo na wanaweza,na hiyo yote ni kwasababu ya kuweza kuwamiliki ambao wanaweza kuwa lipa kile kidogo walichonacho”.Alisema.

Rapper huyo ameongeza kuwa wasanii wapya hawajui thamani yao tofauti na wasanii wakongwe kama yeye wanaojitambua.






Credit:Bongo5.

KOVA:MHE.KAPUYA HANA KOSA LA KUHOJIWA NI MAMBO YAKE BINAFSI.


Akiongea na Wanahabari mchana leo,kamanda Kova amesema,hawezi kumuita Mhe.Kapuya kwasababu haya ni mambo yake binafsi na hakuna mtu yeyote amekuja hapa polisi kulalamika kutendewa vibaya na Mheshimiwa Kapuya.

“Hata hivyo kamanda Kova amesema,kama kuna ushahidi wowote wa kueleweka sio kusingizia mtu vituo vya Polisi viko wazi masaa 24.”

AIBU:HUYU DADA STAR WA KENYA NOUMA SANA.ATUNDIKA PICHA ZINGINE AKIWA NUSU UCHI.


Huyu dada Kiboko Ajali mtu na si kwamba hizi picha zimevuja ama laa!....Bidada huyu kajipiga mwenyewe kwa raha zake na kuzitundika mtandaoni.

Hapo akiwa mjini Bangkok kwa mapumziko.

KUMBE HICHI NDICHO ANACHOPENDA HUYU MSANII WA KIKE KUTOKA THT.MMMMH HATARI.


MWANAMUZIKI,Linah Sanga,ameweka wazi kitu ambacho anakipenda katika maisha yake ukiachilia mbali na muziki anaopiga. Unajuwa ni kitu gani hicho?. Ni viatu.

Akizungumza na MwanaSport,Lina anasema anapenda viatu kuliko kitu kingine kiasi kwamba anaweza kushuka kwenye gari sehemu yoyote kama ameona kiatu kizuri dukani.

Amesema kuwa hata kama akivaa nguo ya siku nyingi kiasi gani,lakini miguuni kama amevaa kiatu kipya hujisikia huru na mwenye furaha,kuliko akikosa kiatu anachokipenda.

Amesema kuwa chumbani kwake anajozi 50 ya viatu anavyovivaa,lakini pia anajozi 30 za viatu ambavyo bado hajavivaa kabisa kwani anatafuta nguo za kuvalia viatu hivyo.

“Yaani hapa bado kabisa.Ninaongeza viatu karibu kila siku maana ninavyoviona madukani vipo vya kila aina nami napenda sana viatu,” Anasema.

Aliongeza kuwa hajawahi kuishi bila kutamani kununua kiatu ambacho amekiona mahali na kila akinunua anakutana na kingine,hivyo ameishi akinunua viatu bila kujali idadi ya alivyonavyo.

Kwa upande mwingine, Lina anasema kama akiambiwa achaguwe kusafiri,kuangalia runninga na kusoma vitabu, atachagua kusafiri kwa kuwa akiwa safarini atajifunza vitu vingi kwa kuona na si kuhadithiwa.Aidha anasema awapo safarini, husinzia kwa bahati mbaya tu lakini ingekuwa ni uwezo wake asingekuwa anasinzia hata kidogo ili aweze kuona kila kilichopo njiani.

“Kama nimelala safarini ujuwe ni kwa bahati mbaya,lakini mimi mwenyewe huwa sitaki kabisa. Huwa ninataka nione kila kitu cha njiani, ni raha yangu pia,” Anasema.

Anaendelea kueleza baadhi ya vitu anavyopenda katika maisha yake kuwa ni pamoja na kuvaa magauni ya mtindo wowote,iwe ni marefu au mafupi.

Anasema kwa kuwa ana umbo la kuvutia,haoni haja ya kujibana kwa kupenda kuvaa suruli kama walivyo wasichana wengi wa siku hizi.

“Huwa na vaa suruali sikatai,lakini sipendi sana kujibana na ndio maana napenda kuvaa magauni ambayo kama una Shepu nzuri hayana shida.Kwa jinsi nilvyo kila nguo nikivaa naiona sawa kwa kuwa nipo poa,” anasema.

Anafafanua kuwa, siyo kwamba havai nguo nyingine,anavaa kwa kuwa hawezi kuvaa nguo za aina moja kila siku,lakini ili awe huru na kuona amependeza,anaa gauni.






Credit:Mwanaspot.